015
ELIMU YA DINI YA KIISLAMU
(Kwa
Watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)
1.0
UTANGULIZI
Fomati hii ni maboresho ya fomati
ya mwaka 2008 iliyotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania. Fomati hii
inatokana na muhtasari wa Elimu ya Dini ya Kiislamu wa mwaka 2012. Katika
fomati hii, maboresho yamefanyika katika muundo wa mtihani. Badala ya kuwa na
karatasi mbili (015 Elimu ya Dini ya Kiislamu 1 & 2), kutakuwa na karatasi
moja ya somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu. Maboresho haya yamefanyika kutokana
na kujirudia kwa mada
zilizokuwa zikitahiniwa karatasi
ya 1 na ya 2. Aidha katika fomati hii, msisitizo umewekwa kwenye maswali ya umahiri
yanayopima ngazi za juu za kufikiri. Hata hivyo, katika fomati hii hakuna
mabadiliko katika mada zitakazotahiniwa.
2.0
MALENGO YA JUMLA
Mtihani utapima ni kwa kiwango
gani mtahiniwa anaweza:
2.1 kuielezea Dini ya Kiislamu;
2.2 kuchambua Sura zilizoteuliwa
za Qur’an na kueleza uhusiano wake na maisha ya mwanadamu;
2.3 kueleza chimbuko la Fiqh na
Sharia kwa ujumla;
2.4 kuchambua Nguzo za Uislamu na
uhusiano wake na maisha ya kila siku;
2.5 kueleza Nguzo za Imani na
matumizi yake katika kufanya ibada za kila siku; na
2.6 kueleza kwa usahihi Historia
ya Uislamu.
3.0
UJUZI WA JUMLA
Mtihani utapima uwezo wa
mtahiniwa katika:
3.1 kueleza maana, dhima,
ukusanyaji, uhifadhi na mafunzo ya Hadithi na Sunnah;
3.2 kueleza kuhusu kushushwa,
kuhifadhiwa na kukusanywa mafunzo ya Sura zilizochaguliwa;
3.3 kuthibitisha na kuitetea Qur’an
kuwa ni neno la Mwenyezi Mungu;
3.4 kueleza dhana ya Dini ya
Uislamu;
3.5 kuchambua nguzo za imani na
nguzo za Uislamu;
3.6 kutofautisha Uislamu na imani
nyingine;
3.7 kuchambua chimbuko la Fiqh;
3.8 kuhusisha Fiqh na maisha ya
kila siku;
3.9 kueleza mtazamo wa Uislamu
juu ya Ibada;
3.10 kuchambua mfumo wa maisha ya
Kiislamu, Kijamii, Kiuchumi na Kisiasa; na
3.11 kuchambua nyakati muhimu
katika dini ya kiislamu kabla ya Mtume (s.a.w) kipindi cha Mtume (s.a.w),
kipindi cha Makhalifa wa Mtume hadi sasa na maisha ya kila siku ya Waislamu na
zama za sasa.
4.0
MAELEKEZO YA MTIHANI
Mtihani utafanywa kwa muda wa saa
tatu (3). Mtihani utakuwa na karatasi moja (1) iliyogawanyika katika
sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali 13. Mtahiniwa atatakiwa kujibu
jumla ya maswali 12.
Sehemu A itakuwa na
maswali mawili (2). Swali la kwanza litakuwa na vipengele 15 vya
maswali ya kuchagua na swali la pili litakuwa na vipengele vitano (5) vya
maswali ya kuoanisha. Kila kipengele katika maswali yote mawili kitakuwa na
alama moja (1). Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali yote. Sehemu hii
itakuwa na jumla ya alama 20.
Sehemu B itakuwa na
maswali saba (7) ya majibu mafupi. Mtahiniwa atatakiwa kujibu
maswali yote. Kila swali litakuwa na alama tano (5). Sehemu hii itakuwa
na jumla ya alama 35.
Sehemu C itakuwa na jumla
ya maswali manne (4) ya insha. Mtahiniwa atatakiwa kujibu maswali
matatu (3). Kila swali litakuwa na alama 15. Sehemu hii
itakuwa na jumla ya alama 45.
5.0
MAUDHUI YA MTIHANI
Mada zifuatazo zitapimwa katika
mtihani wa somo hili:
5.1 Mtazamo wa Uislamu juu ya
Elimu
5.2 Imani ya Uislamu
5.3 Kumjua Mwenyezi Mungu
5.4 Mtazamo wa Uislamu juu ya
dini
5.5 Fiqh
5.6 Chimbuko la Fiqh
5.7 Mtazamo wa Uislamu juu ya
ibada
5.8 Dini sahihi anayostahiki mwanadamu
5.9 Nguzo za Uislamu
5.10 Mambo ya lazima kufanyiwa
maiti wa Kiislamu
5.11 Nguzo za imani
5.12 Familia ya Kiislamu
5.13 Mfumo wa jamii ya Kiislamu
5.14 Qur’an
5.15 Sunnah na Hadithi
5.16 Historia ya Mitume
walioteuliwa
5.17 Bara la Arab zama za
Jahiliya
5.18 Haki na Uadilifu katika
Uislamu
5.19 Dola ya Kiislamu Madina
5.20 Historia ya Uislamu baada ya
Kutawafu Mtume (s.a.w) hadi hivi leo